Sunday, December 25, 2011

sikutoa track ya 'riz one' kwa lengo la kutaafuta imaarufu-izzo b

 
MSANII wa muziki wa kizazi kipya aliyeimba wimbo wa ‘Riz One’, Izzo Business, amefunguka na kusema kuwa tangu atoe kazi hiyo hakuna majibu yoyote aliyoyapata kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwani hakutoa kazi hiyo kwa lengo la kutafuta umaarufu zaidi ya kutoa kero za Watanzania ambao ndiyo wanaoumia.

Akizungumza na mtandoa wa Burudani wa DarTalk, Izzo  alisema baada ya kutoa wimbo alitumai angeweza kukutana na Rais lakini hakuna kitu chochote kichofanyika ingawa anaamini kazi hiyo wamesikiliza na wamejua nini kinachoongelewa.

Alisema mambo yote aliyoyaimba yapo katika taifa la Tanzania lakini anashangaa haoni mabadiliko yoyote kutoka Serikalini huku watanzania wakizidi kuumia na upandishwaji wa bei ya vyakula, rushwa na vitu vingine vingi vinavyokwamisha maendeleo.

“Unajua wasidhani kwamba nimetoa wimbo ule kwa lengo la kutafuta umaarufu hapana mimi nawakilisha jamii hivyo mambo yote ambayo nimezungumza mle ndani yapo na yanasababisha wananchi wazidi kuwa maskini.” alisema.

Hata hivyo msanii huyo alisema kuwa suala la dawa za kulevya hivi sasa limekuwa sungu na linazidi kuwamaliza vijana na hayo yanatoka nje ya nchi lakini cha kushangaza yanapita bandarini na hakuna siku ambayo Serikali imetangaza kuna mzingo wa dawa la kulevya umekatwa bandarini.

Alisema wimbo huo ulikuwa mahususi kwa mtoto wa Rais ili afikishe ujumbe kwa baba yake sababu yeye anapata muda mwingi wa kuzungumza naye kama kijana ambaye anaweza kumshauri baba yake jua masuala hayo katika kusaidia taifa hili ingawa yapo baadhi ya mambo amefanya vizuri.

No comments:

Post a Comment