Sunday, December 4, 2011

SITARAJII KUTOA ALBUM TENA – SOGGY

Msanii wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini kutoka kundi la Hot Pot Family, Soggy Doggy asema, ‘’sitarajii kutoa albam kutokana na gharama za kuiandaa kua kubwa na pindi iwapo sokoni faida haionekani kwani wahindi wanatunyonya’’. Msanii huyu alitamba na nyimbo zake za awali kama vile “Kibanda cha simu”, “Nilikaona mwaka jana” pamoja na “Nimchague nani”, zinazopatikana kwenye albam zake tatu alizowahi kuzifanya kipindi cha nyuma.

Kwa sasa Soggy anatarajia kuachia nyimbo yake mpya hivi karibuni ambayo ipo mikononi mwa produza P.Funky Majani katika studio za Bongo Records, hivyo mashabiki wa Soggy Doggy pamoja na Hotpot Family mnaombwa kukaa tayari kuipokea kazi hiyo mpya.

No comments:

Post a Comment