Sunday, November 20, 2011

FILAMU JAMVINI

Jee ni Video au Filamu ?
    Japo nimeazimia kuongelea juu ya swala la uwigizaji na utengenezaji wa picha naona ni vyema kwanza nikaongelea juu ya video na filamu kabla sijaingia kwa undani Juu ya swala zima la hatua za utengenezaji wa picha.Kuna mgongano mkubwa katika swala zima la lugha fasaha ya picha hizi, Wengine huita Video na wengine huita Filamu. Ukweli ni kwamba yote yana maana moja, tafauti ipo katika utayarishaji kwa kuzingatia ubora na gharama.Iwe Video au iwe Film zote hizi ni picha,picha zenye nyendo/kutembe (Motion picture au Movie).
 Watu wa makamu kidogo watakumbuka enzi zile za kununua mikanda ya picha za kawaida (still picture) mikanda hii ilikua katika mfumo wa filamu (film), kulikuwa na film zenye nembo za Olympic,Agfa,Kodak, Fuji n.k. Mikanda hii (kwa uchache wake) mingine mpaka leo inauzwa katika baadhi ya studio. Na hivyo ndivyo ilivyo katika swala la sinema pia. Mpaka leo hii mikanda(filamu) ya 16 MM, 36 MM 35MM bado ipo katika soko la sinema.  Matumizi ya Filamu ya sifika kwa ubora wake, tatizo ni gharama ya kupiga picha (kurekodi) na halafu kuhariri kwa kukata kata.Wakati mwingine inabidi pia kuhariri mkanda wa sauti peke yake na kisha kuoanisha sauti na picha kwa pamoja(synchronization). Kwa sasa tekinolojia imekua sana na filamu hizi hizi zimeboreshwa na inawezekana kurekodi picha na sauti kwa pamoja. Haya yato yahitaji muda mwingi na muda ni mali na ni ghali pia. THANKS NURU YA KALAMU

No comments:

Post a Comment